Alhamisi , 14th Sep , 2017

Polisi mkoani Geita wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliofunga barabara kuelekea kwenye mgodi wa GGM.

Tukio hilo limetokea mapema leo ambapo pia madiwani wa eneo hilo na baadhi ya wananchi wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema bado hali ni tete, hivyo atatoa taarifa rasmi baada ya kuhakikisha hali ya kiusalama imetulia mgodini.

Leo asubuhi wananchi wa mkoa wa Geita wamefunga barabara inayoingia katika mgodi wa GGM kushinikiza malipo ya kodi ya dola 12.