Daisy Korir - Mhazini wa KMPDU, akizungumza na wanahabari baada ya kutoka gerezani
Viongozi hao saba walifungwa Jumatatu wiki hii baada ya kupatikana na hatia ya kutotii amri ya mahakama ya kuwataka kumaliza mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa zaidi ya miezi miwili sasa.
Viongozi hao wametakiwa kuhakikisha suluhu ya mgomo huo inapatikana katika kipindi cha siku saba.
Mazungumzo ya kutafuta suluhu yataongozwa na Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) na Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (KNHCR).
Madaktari wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara na kuboresha mazingira ya utendaji kazi hospitalini
Wamekataa mshahara walioongezewa na serikali wa asilimia 40 wakisema kuwa ni wa chini kuliko ule walioafikiana mwaka 2013.