Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Watuhumiwa 11 wa kesi ya mauaji ya mwanaharakati mpinga ujangili wa Tembo, Wayne Lotter aliyeuawa Masaki jijini Dar es Salaam siku ya Agosti 16, 2017, wamehukumiwa kunyongwa baada ya Mahakama kuwakuta na hatia.

Waliohukumiwa kunyongwa kutokana na mauaji ya Wayne Lotter

Hukumu hiyo imesomwa leo Desemba 2, 2022, na Jaji Leila Mgonye wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, ambapo amebinisha kuwa watu hao waliohukumiwa wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. 

Watu waliohukiwa ni wanaume 10 na mwanamke mmoja, ambao wanaume hao 10 wamepelekwa Gereza la Ukonga na Mwanamke akipelekwa Gereza za Segerea.

Wayne ambaye alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, taasisi ambayo ilikuwa mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini Tanzania aliuawa  Agosti 16, 2017 wakati akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akielekea nyumbani kwake Masaki.

Wayne Lotter aliyeuawa mwaka 2017