Alhamisi , 14th Oct , 2021

Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kwa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kwamba katika kuhitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022, wahakikishe hakuna dosari itakayojitokeza kwenye miradi yote itakayokaguliwa na kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ndani ya maeneo yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Chato, Geita, wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, ambapo imebainika kwamba kuna jumla ya miradi ya bilioni 15.3 ambayo imekataliwa na Mwenge huo kwa kuwa haikukidhi viwango vinavyotakiwa.

"Niwatake viongozi wa maeneo, tunapozima Mwenge mwakani idadi ya miradi yenye dosari ipungue sana, na kwa ile mikoa ambayo bado itajitokeza ina miradi yenye dosari tutaelewano wakati huo, hili ni onyo kwa wakuu wa mikoa na wialaya na wakurugenzi," amesema Rais Samia