Jumanne , 29th Sep , 2015

Wakurugenzi watendaji wa halmashauri za mikoa ya Njombe na Ruvuma wameiomba serikali kuwawekea ulinzi wa kutosha wakati wa uchaguzi ili kulinda maisha yao baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Katibu tawala wa mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu

Hayo yamebainishwa katika semina ya siku mbili ya kuwakumbusha wakurugenzi na wasimamizi wa uchaguzi kwa ngazi ya wilaya wa halmashauri za mikoa ya Ruvuma na Njombe kwa kanda ya nyanda za juu Kusini yaliyoendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC mwishoni kwa wiki hii.

Wakurugenzi hao wameomba ulinzi wakati wa kuanza uchaguzi na baada ya kutangaza matokeo kwa muda ili kuwaweka salama kwa kuwa matokeo ya uchaguzi yanakuwa yameumiza upande fulani kwa kuwa kuna ushindi na upande utashindwa.

Akiuliza swali kwa tume ya uchaguzi taifa NEC Mkurugenzi wa halmashauri ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Ally Mpenye, amesema kuwa wamekuwa na wasiwasi wakati wa kutangaza matokeo hivyo tume na serikali kwa ujumla ihakikishe kuwa watumishi na wahusika wa utangazaji wa matokeo wanahakikishije ulinzi wa kutosha wakati wote wa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa wa uchaguzi Kanda ya nyanda za juu Kusini Jane Tungu amesema kuwa tume ratiba yake inasema kuwa kuna vifaa vina wahi katika vituo lakini kama karatasi za kupigia kura hazina haja ya kuwahi kufika katika vituo ndio maana zinapelekwa siku moja kabla ya kupiga kura.

Kwa upande wake mgeni rasmi aliyefungua semina hiyo Katibu tawala wa mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Rehema Nchimbi amesema wasimamizo wakakikishe kuwa hawafanyi kazi kwa mazoea bali wafanye kazi hiyo kwa uzoefu wa kuelewa kanuni za uchaguzi.