Jumamosi , 10th Dec , 2016

Wafanyabiashara wa mchele katika soko la Mapinduzi lililopo Mwananyamala Jijini Dar es Salaam wameahidi kutopandisha bei ya mchele katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kama ilivyo katika masoko mengine

Wamesema badala ya kupandisha bei ya mchele sokoni hapo, itaendelea kushuka siku hadi siku.

Wakizungumza na Hotmix iliyotembelea sokoni hapo jana, wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa mchele sokoni hapo unauzwa kwa bei ya chini ya hadi shilingi elfu moja kwa kilo; na hii yote ni kwa ajili ya kuwajali wateja wao ambao wengi wao wana hali duni ya kifedha.

Wamesema kuwa hatua yao hiyo inatokana na ukweli kwamba soko hilo linaundwa na wafanyabiashara ambao wakulima na kwamba katika baadhi ya siku, huamua kuuza mchele kwa bei ya kutupa ya hadi shilingi mia tatu kwa kilo moja ili kuwaonesha wateja wao kwamba wanawajali.