Jumatano , 23rd Aug , 2017

Baadhi ya wabunge wapya nchini Kenya wamepinga mpango wa kupunguza mishahara yao kwa asilimia 15 kulingana na tarifa iliyosambaa kupitia mtandao wa Twitter wa chombo kimoja cha runinga.

Hatua ya kupunguza mshahara huo inayoshirikisha marupurupu kadhaa ilitarajiwa kuanza kutekelezwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti nane.

Mnamo mwezi Juni, Tume ya Marupurupu na Mishahara nchini humo ilisema kuwa mpango huo umelenga kupunguza mishahara ya wafanyakazi wa serikali kwa asilimia 35.

Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa Wabunge wanaolipwa mishahara ya juu duniani, na hatua ya kuipunguza mishahara hiyo ni mojwapo ya mipango ya serikali kupunguza mishahara ya wafanyakazi wa serikali.