Jumamosi , 3rd Dec , 2022

Wakazi wa kata ya Mwaduilohumbo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambao nyumba zao na mashamba yalifunikwa na tope, baada ya bwawa la maji machafu katika mgodi wa Williamson Diamond kupasuka na kusambaa kwenye makazi ya watu, wameiomba serikali kuharakisha  tathimini ili walipwe fidia.

Christina Juma, mkazi wa Mwaduilohumbo

Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwangolo Kata ya Mwaduilohumbo ambao baadhi yao mashamba na nyumba zao zimejaa tope, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu wakati zoezi la tathimini likiendelea huku akiwataka kutoa taarifa sahihi.

Kwa upande wake Afisa uhusiano na jamii Bernard Mihayo kutoka mgodi wa Williamson Diamond amesema wanaendelea kutoa msaada wa chakula na kulipia gharama za kupanga nyumba kwa waathirika.

Bwawa la maji machafu la mgodi wa Mwadui lilipasuka Novemba 7 mwaka huu na tope kusambaa kwenye makazi ya watu ambapo kaya zaidi ya 30 zenye wakazi 145 waliathirika.