Jumapili , 17th Sep , 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali wasiokuwa na mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Septemba, 17 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga.

“Kama huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo,”

Amesema kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao Serikali inahamasisha watu wafungue mashamba mapya nao watumie fursa hiyo na kulima.

Amesema ni vema kila mdau akahahakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo kama ni mkulima alime kwa kuzingatia stadi za kilimo na mnunuzi azingatie taratibu zilizopo.