Jumamosi , 31st Oct , 2020

Baadhi ya viongozi wa kiroho mkoani Dodoma wamewashauri wagombea wa nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, na matokeo ya mshindi wa urais kutangazwa jana Oktoba 30, kuhakikisha wanaridhika na matokeo waliyoyapata na kushirikiana katika kujenga nchi.

Askofu wa makanisa ya Philadelphia Gospel Assembly, Dkt. Yohana Masinga.

Akizungumza na East Africa Television Askofu Mkuu wa Makanisa ya Philadelphia Gospel Assembly, lenye makao makuu yake jijini Dodoma Dkt. Yohana Masinga, amesema wagombea walioshindwa wasikate tamaa kwani wanatakiwa kujaribu kipindi kijacho.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la AGT Ipagala Dkt. Evance Chande, amesema kuwa wagombea walioshindwa ni kutokana na kile walichopanda kwa wananchi na hivyo amewaomba washirikiane na washindi.