Jumatatu , 17th Jul , 2017

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dr.Jakaya Kikwete ameongoza waombolezaji kutoa salamu za pole kwa familia ya Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr.Harison Mwakyembe nakusema anamkumbuka marehemu Lina Mwakyembe kwa uchapakazi na ushirikiano

Dkt. Kikwete amesema hayo muda mchache alipowasili nyumbani kwa Mwakyembe Kunduchi Jijini Dar es Salaam ambapo shughuli za mazishi zinafanyika kabla ya kuondoka kuelekea mkoani Mbeya kwa maziko siku ya kesho (Jumanne).

"Nimekuja kumpa pole Harrison, tunafahamiana muda mrefu na mkewe alipokuwa anaugua pale Muhimbili nilikuwa naenda kumtembelea lakini juzi nilivyokuwa kijijini ndiyo nimepata taarifa za mama yetu ametutoka. Ni msiba wetu sote tunaelewa majonzi yake, uchungu aliyokuwa nao yeye na familia yake lakini kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu kinapotokea sote ni tunatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu", amesema Mzee Kikwete.

Aidha, viongozi wengine tofauti na Mzee Kikwete walioweza kufika na kutoa salamu zao pole ni pamoja na Spika wa Bunge Mstafu Anna Makinda, Waziri wa  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji, DPP Biswalo Mganga, Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Uchaguzi NEC Jaji Damian Lubuva na viongozi wengine kutoka kwenye Taasisi na Nchi mbal;imbali walifika.

Kwa upande mwingine, ratiba ya kuaga mwili wa marehemu itafanyika kesho kama ilivyopangwa katika kanisa la KKT Kunduchi  na kuagwa nyumbani Kunduchi wakiongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mtazame hapa Mzee Kikwete akitoa salamu zake.