Jumamosi , 21st Oct , 2017

Nchini Malawi kumekua na taarifa za kuwepo kwa watu wanaonyonya damu (vempire) na kuibua hali ya hofu kwa wakazi wa nchi hiyo hasa wanaoishi vijijini, huku kukiwa na vurugu kubwa zinazosababisha mauaji ya watu.

Matukio hayo yaliibuka mwezi Septemba ambapo baadhi ya watu akiwemo mmoja wa wabunge nchini humo, kuthibitisha kuwepo kwa wanyonya damu hao wanaohusishwa na imani za kishirikina, akieleza kwamba watu hao wana vyuma ambavyo watu wakiviangalia hupoteza nguvu.

Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika amewataka wananchi kuacha mara moja vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kuua watu, huku akiwaonya wanyonya damu hao kuacha mara moja matendo hayo ya imani za kishirikina, na atapambana nao akisema vimeisikitisha serikali ya nchi hiyo.

Kufuatia vitendo hivyo watu 8 mpaka sasa wameuawa kwa kupigwa na makundi ya watu, wakiwahusisha na vitendo vya unyonyaji damu, huku mmoja wao akichomolewa kwenye kituo cha polisi alikowekwa na kupigwa mawe na wananchi mpaka kufa.

Nao Umoja wa Mataifa umeondoa baadhi ya wafanyakazi wake kwenye maeneo ambayo yana vurugu zaidi, na kuwaamuru kuhamia sehemu salama zaidi.

Matukio ya vitendo vya unyonyaji damu yaliwahi kuibuka mwaka 2002, huku yakihusishwa na ushirikina kutoka nchi acheter du cialis en ligne jirani ya Msumbiji.

Imetafsiriwa kutokaVOA & BBC