Jumapili , 19th Feb , 2017

Kuanzia sasa, kwa mtu yeyote atakayekutwa na shamba la dawa za kulevya aina ya banngi, anaweza kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha kuanzia miaka 30 gerezani

Shamba la bangi tayari kwa kuteketezwa, huku mtuhumiwa wa kilimo hicho akiwa chini ya ulinzi (Picha: Maktaba)

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya, ambayo imeanza kutekelezwa hivi karibuni.

Mbali na adhabu hiyo, sheria hiyo pia imeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu atakayebainika kusafirisha aina yoyote ya dawa za kulevya, pamoja na wale wanaoingiza dawa kutoka nje ya nchi.

Pia sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya shilingi milioni 200 na kifungo cha maisha kwa watakaokutwa na malighafi au maabara za kutengezea dawa za kulevya huku ikiweka adhabu ya kifungo cha miaka mitano na/au faini ya kuanzia shilingi milioni moja kwa mtu atakayekutwa na kiasi kidogo cha dawa cha dawa za kulevya.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe, akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, kwa ajili ya uchambuzi wa sheria hiyo mpya, ambapo pia ameelezea utofauti wa sheria hiyo ya mwaka 2015 na ile iliyokuwepo ya mwaka 1995.

Dkt Harrison Mwakyembe

Amesema lazima kutakuwa na ukosoaji kwa kuwa sheria hiyo ni mpya hsa katika suala la mashahidi, lakini kuna sheria nyingine ya kulinda mashahidi (Whistle Blowers Act), ambayo itasaidia kuwalinda watu wanaotoa taarifa kuhusu wahusika wa dawa za kulevya

Amesema pia serikali iko tayari kupokea maoni kutoka kwa wadau, juu ya nini kifanyike ili kuwadhibiti wahusika wa dawa za kulevya ambao wamekuwa wakiifanyia wema jamii inayowazunguka kwa kiasi kikubwa.

Huyu hapa Dkt Mwakyembe akifafanua