Jumapili , 17th Sep , 2017

Serikali ya Kenya imetangaza kupunguza matumizi katika baadhi ya taasisi za serikali ili kupata fedha kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa marudio wa Urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 17.

Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Henry Rotich, amesema, tume mbalimbali pamoja na County zote 47 zitaathirika na uamuzi huo wa kubana matumizi.

Bw. Rotich amesema tayari wametangaza kupiga marufuku safari za nje kwa maafisa wa serikali bila ya kibali maalum kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Uchaguzi huo wa marudio unatarajia kuligharimu taifa hilo la Afrika Mashariki Dola za Kimarekani milioni 150, na kwamba serikali haitarajii kukopa fedha nje kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi huo.