Jumatatu , 7th Sep , 2020

Tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2020 zimechelewa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababisha homa ya mapafu wa Covid 19 ambao ulisababisha kuzuia mikusanyiko.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Kufuatia mlipuko huo sherehe hizo ziliahirishwa mara mbili ambayo pia imesababisha changamoto katika ukusanyaji wa rasilimali fedha.

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga wakati wa kuwaapisha majaji watakaozipitia kazi ziizowasilishwa kwaajili ya kushindanishwa.

“Jumla ya kazi 450 zimewasilishwa kushindanishwa katika makundi 21 ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2019”, amesema Kajubi.

Akizungumza baada ya kuwaapisha majaji wateule, mwenyekiti wa kamati ya maadili ya MCT, Jaji Mstaafu Juxon Mlay amewataka kufanya kazi hiyo kwa uadilifu ili kuwe na ushindani utakaoleta tija katika tasnia ya Uandishi wa Habari.