Jumanne , 23rd Mei , 2017

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka na kuwataka vijana wadogo wanaojihusisha na matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha waache mara moja kwani jeshi la polisi halitawaacha salama.

Kamishna Simon Sirro

 

Sirro amesema hayo jana wakati akitoa rai kwa majambazi na kusema Dar es Salaam ni sehemu nzuri ya kuishi na kuwataka majambazi kuacha mara moja kazi hiyo kama wanazipenda familia zao.

"Nipeleke salamu kwa majambazi Dar es Salam ni sehemu nzuri sana ya kuishi lakini kama unapenda sana familia yako, maana najua wengi wana familia, hii biashara ya bunduki hailipi hata kidogo, acha biashara ya bunduki fanya kazi zingine maana mwisho wa siku tunakuhitaji na tutakukosa, ukiangalia hawa walioondoka ni watoto wadogo ukianza haya mambo na miaka 24 au 30 mambo ya bunduki haitakusaidia sana acha hiyo biashara na kama una vibunduki vyako vitupe barabarani" alisema Sirro 

Sirro aliendelea kusisitiza 

"Ni bora ufanye hata kazi nyingine, fanya biashara ya bodaboda, fanya biashara ya kuuza nyanya italipa zaidi kuliko hii kazi ya ujambazi ambayo wanajiingiza" alisema Sirro