Alhamisi , 25th Aug , 2016

Tetemeko lingine la ardhi lenye ukubwa wa rishta 6.8 limekumba mkoa wa kati wa Myanmar.

Tetemeko la Ardhi Myanmar

Watu watatu wameripotiwa kufariki katika tetemeko hilo ambalo lilisikika hadi mji wa Bangkok nchini Thailand na Dhaka nchini Bangladesh.

Ndugu wawili wamekufa kwenye maporomoko yaliyosababishwa na tetemeko hilo nchini humo.

Zaidi ya watu elfu moja waliokuwa wanasherehekea sherehe za kibudha wameathiriwa na tetemeko hilo.