Ijumaa , 15th Jan , 2016

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imezima mitambo iliyokuwa ikitumiwa na Six Telecom Tanzania LTD, kwa kukiuka kanuni na taratibu za leseni za mawasiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Rashid Shamte

Kwa mujibu wa mlaka hiyo imesema kuwa ukiukwaji huo wa sheria uliofanywa na kampuni hiyo umeisabishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 8 za kitanzania.

Akizungumza mara baada ya kuifunga mitambo hiyo mwanasheria kutoka mamlaka hiyo ya mawasiliano amesema kuwa operesheni hiyo ni mwazo tu wa kuayapitia makampuni ya mawasiliano yanayokiuka sheria na kuwaibia wananchi.

Akizungumza mara baada ya mashine zote za kampuni hiyo kuzimwa mkurugenzi wa kampuni hiyo bw, Rashid Shamte ameitupia lawama TCRA kwa kushindwa kuhakikisha kuwa bei elekezi kwa simu kutoka nje inasimamiwa kikamilifu.