Ijumaa , 5th Jun , 2015

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA imesema itaendelea kutoa elimu kwa makundi yote yenye mahitaji maalum hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha yanapata huduma za mawasiliano bila ya kubaguliwa.

Mkurugenzi wa idara ya watumiaji na watoa huduma za mawasiliano kutoka TCRA Dkt. Raymond Mfungahama amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati TCRA ilipokutana na jamii ya watu wasiona kwa lengo la kuwapa elimu ya namna ya matumizi bora ya mitandao.

Dkt. Raymond amesema elimu wanayopewa kundi hilo haina tofauti na ile wanayopewa watu wengine hivyo ni wajibu wa wananchi kutambua kwamba kila kundi lina haki zake za kimsingi na kisheria.

Amesema kundi la watu wenye ulemavu lina nafasi yake katika jamii lina haki kama ilivyo kwa wengine ya kupata habari kupitia njia yoyote ya mawasiliano hivyo ni wajibu wa TCRA kutoa elimu kama hiyo ili kuelewa namna watakavyoshiriki kupata habari kwa njia ya mitandao