Ijumaa , 30th Mei , 2014

Raia watatu wa Kenya na Mtanzania mmoja jana wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutoa huduma ya mawasiliano ya simu za kimataifa pasipo idhini ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.

Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma.

Afisa Habari wa TCRA Doris Saivoiye amesema watuhumiwa hao wametenda kosa hilo kwa kipindi cha wiki moja ambapo wameisababishia TCRA hasara ya fedha taslimu shilingi milioni 173.

Bi. Saivoiye pamoja na mhandisi mwandamizi wa TCRA Mwesiga Wilson Barongo, wamezungumzia jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa ambao hivi sasa wapo rumande kutokana na hakimu anayesikiliza shauri lao kuwa na udhuru.