Jumapili , 17th Sep , 2017

Serikali ya Brazil imeisamehe serikali ya Tanzania deni lenye thamani ya bilioni 445 za kitanzania, ililokuwa inadaiwa na nchi hiyo.

Tarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas kwenye ukurasa wake wa twitter, na kufafanua kwamba deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma, mwaka 1979 pamoja riba yake.

"Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya dola za Kimarekani mil. 203 ambazo ni sawa na tsh bil. 445,deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja riba," ameandika Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas

Msemaji wa serikali ameendelea kwa kusema kwamba kitendo hicho kimefungua milango iliyokuwa imefungwa kutokana na deni hilo, ambapo sasa makampuni ya Brazil yataweza kuja nchini na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Pia serikali imeshukuru Brazil kwa kitendo hicho na kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kuleta maendeleo ya nchi.

alichokiandika Msemaji wa serikali twitter