Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Shule ya msingi Laalakir iliyopo kijiji cha Partimbo kata ya Partimbo wilayani Kiteto mkoani Manyara, imekuwa na matokeo ya alama "A" kwa miaka 10 mfululizo na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa na haijawahi kufelisha mwanafunzi

Wanafunzi waliofanya mtihani  mwaka huu 2022 ni 36, kati ya hao 35 wamepata alama A na B mmoja.

Shule hii ilijengwa na watu wa Jamhuri ya China kati ya shule tatu zilizojengwa, Tanzania Bara na Visiwani, moja ilijengwa Kiteto Manyara, nyingine Mkoa wa  Pwani na moja Zanzibar