Serikali yatoa Miezi 3 kwa wananchi

Monday , 13th Nov , 2017

Wanakijiji 1,830 wa kijiji cha Bwila Chini Mkoani Morogoro wapewa miezi mitatu kuhama Wananchi zaidi ya 1,800 wa kijiji cha Bwila Chini na Kiburumo tarafa ya Mvuha Wilaya ya Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen

Wakazi hao wametakiwa kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi hicho kwa ajili ya kupisha ujenzi wa bwawa katika eneo hilo baada ya kulipwa fedha zao za fidia na kumalizika kwa msimu wa Mavuno.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa malipo ya fidia awamu ya pili katika viwanja vya Shule ya Msingi Bwila Chini, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe, amesema lengo la Serikali ni kutaka wananchi hao kupata makazi mapya baada ya kutakiwa kupisha ujenzi wa bwawa katika eneo hilo hivyo ni vyema wakatumia kiasi hicho cha fedha kama ilivyoelekezwa.

Kwa upande wake, Meneja Miundombinu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Morogoro ,Mhandisi John Kirecha, amesema, malipo hayo yanatokana na malalamiko yaliyoibuka wakati wa malipo ya awamu ya kwanza mwaka 2014 ambapo jumla ya shilingi Bilion 4 zinatarajiwa kulipwa kwa wananchi zaidi ya 1,800.