Ijumaa , 21st Oct , 2016

Serikali imeongeza muda wa usajili wa vitambulisho vya taifa kwa watumishi wa umma, na kutoa onyo kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya umma watakaoshindwa kusimamia zoezi hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba.

 

Uamuzi huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba, kwa pamoja na Waziri wa Nchi Utumishi na Utawala Bora Angela Kairuki wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Waziri Nchemba amesema kuwa watumishi waliokosa baadhi ya nyaraka wamepewa muda wa siku 14 kukamilisha utaratibu wa kutafuta nyaraka hizo ili kufanikisha zoezi hilo huku akisema kuongeza muda huko kunatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu huo wa baadhi ya nyaraka.

Kwa upande wake Mhe. Angela Kairuki ametoa onyo kwa viongozi watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo ambalo limepangwa kufanyika kwa nchi nzima.