Alhamisi , 17th Aug , 2017

Serikali ya Zimbabwe imemuombea Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe  kinga ya kidplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.

Rais Mugabe akiwa na mkewe Grace Mugabe

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maofisa wa polisi wa taifa hilo leo asubuhi zimedai kuwa hayo yamefanyika kwa mujibu wa sheria, huku wakisisitiza kwamba mwana mama huyo bado yupo Afrika ya Kusini huku wakipinga ripoti za awali zilizosambaa kwamba Grace Mugabe alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.

Hata hivyo Bi Mugabe alitarajiwa kwenda kujisalimisha mwenyewe polisi siku ya Jumanne lakini pia hakufanya hivyo. 

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema, Kaimu Mkuu wa Polisi Lesetja Mothiba (Afrika Kusini) alisema kuwa Grace Mugabe anatakiwa aende mahakamani kulingana na sheria.

Taarifa za awali zinasema kuwa Bi Mugabe anadaiwa kutenda kosa la kumshambulia mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 katika hoteli jijini Johannesburg Afrika ya Kusini.