Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Kundi la makampuni ya Uniccon limesema kuwa leo Desemba 2, 2022, nchini Nigeria litazindua roboti ya kwanza barani Afrika yenye sura ya binadamu inayoitwa Omeife, na kwamba miongoni mwa lugha zitakazotumiwa na roboti huyo ipo lugha ya Kiswahili.

Roboti Omeife atakayezinduliwa leo

Mkurugenzi Mtendaji wa kikundi hicho, Chuks Ekwueme, ambaye alitangaza hayo katika taarifa yake jana mjini Abuja, alisema hafla hiyo itafanyika leo siku ya Ijumaa.

Ekwueme alisema roboti huyo wa kike wa Kiafrika mwenye urefu wa futi sita anazungumza lugha kama huduma kwa biashara zinazohitaji kuunganisha watazamaji asilia wa Kiafrika, akiongeza kuwa ni roboti ya kazi nyingi na msaada.

"Inawatambulisha wanadamu kupitia sura, ikizingatia kitu mahususi inapohitajika, inatambua vitu, inajua sifa zao na pia inakokotoa nafasi na umbali wa vitu inachokiona, inazingatia mtu maalum kuweka mazungumzo hai," amesema Mkurugenzi wa kampuni hiyo

Roboti hiyo inazungumza lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, na pia lugha za Kiafrika, kama vile Kiswahili, Pidgin, Wazobia, Afrikaans na Igbo.

Jina Omeife ni la Kiigbo linalomaanisha "uwezo wa kufanya mambo mengi".