Jumapili , 4th Dec , 2022

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt Samia, amekuwa akipigiwa mfano na mashirika ya fedha ya kimataifa na nchi mbalimbali duniani kwa ubunifu mkubwa wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotokana na fedha za mkopo usiokuwa na riba wa Benki ya Dunia wa Tril 1.3.

Waziri wa Fedha na Mipano, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Kaselya,

Kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na changamoto ya UVIKO 19.

Hayo ameyabainisha baada ya wakazi wa Kata ya Kaselya, wilayani Iramba mkoani Singida, kuondokana na adha ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kaselya uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 770.

Wakazi hao wameishukuru serikali kwa kufanikisha na kukamilisha ujenzi wa mradi huo, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, alipotembelea na kukagua mradi huo ambao fedha zake zinatokana na mradi wa kukabiliana na athari za UVIKO 19.

"Tunakuomba utupelekee salamu nyingi kwa Rais Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kututatulia changamoto ya maji kafika Kata yetu, ametutua ndoo kichwani wanawake na wewe Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wetu kwa jitihada zako za kufanikisha mradi huu na miradi mingine," walisema wakazi wa kata hiyo

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameahidi kumfikishia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pongezi za wananchi hao kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo kwa kasi kubwa.

Akiwa jimboni, Dkt. Nchemba ametembelea na kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya madarasa  ya shule ya sekondari Ndulungu, kituo cha afya Mwandegembe, shule ya sekondari Mbelekese, kituo cha afya Urugu na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika tarafa ya Ndago.