Alhamisi , 25th Aug , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Andrew Willison Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

Rais wa Tanzania, Dkt John Magufuli

Uteuzi huo umefanyika leo ambapo kabla ya uteuzi huo Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Aidha Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo uteuzi wa Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.