Jumamosi , 25th Mar , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,amemteua Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Rais Magufuli

Kabla ya Uteuzi huo Bw. Charles Edward Kichere alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Bw. Charles Edward Kichere anachukua nafasi ya Bw. Alphayo Kidata ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.
Kufuatia uteuzi huo, nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA itajazwa baadaye.