Alhamisi , 16th Nov , 2017

Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amemsifu na kukiri kwamba Rais Magufuli ni kiongozi mwenye ushawishi kwa mataifa mengine ndiyo maana Mfalme wa Morrocco aliahidi kujenga uwanja wa mpira mkoani Dodoma.

Mh. Shonza ametoa sifa hizo kwa Rais Magufuli wakati akijibu swali la Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ambaye aliuliza ni kwa nini serikali isiteue kati ya Mkoa wa Dodoma au Singida kuwa mji wa pili utakaoweza kuendesha mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika nchini mwaka 2019.

Katika maswali aliyoyauliza Mh. Kingu alikuwa akitaka kujua kama tayari kuna mji wa pili umeshachaguliwa kuendesha mashindano hayo baada ya Dar es salaam kuwa wa kwanza kuteuliwa.

                                                 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu 

Aidha Mh. Kingu akiinadi mikoa aliyoipendekeza ameisifu kwa kusema kwamba kwa sasa Mkoa wa Singida una hoteli za kisasa za kuwamudu wageni mbalimbali pamoja na kiwanja cha mpira cha kisasa kilichikarabatiwa vizuri na Mkoa wa Dodoma ni Mkao Makuu ya nchi na kwamba Rais na viongozi wakuu pia watahamia huko.

Hata hivyo Majibu ya Serikali yaliyotolewa na Mh. Shonza ameka wazi kwamba zipo kamati zilizoundwa kufanya utafiti wa mikoa hivyo ataupendekeza mkoa wa Singida ufanyiwe utafiti kama utakidhi matakwa.

"Moja ya vigezo tunavyozingatia ni uwanja unaokidhi kiwango cha kimataifa na hoteli itakayoweza kuwa-accomodate' wageni watakaokuwepo, lakini kwa upande wa Dodoma nimpongeze Rais wetu kwa ushawishi kwa mfalme wa Morroco kujenga uwanja wa michezo Dodoma" Shonza

Ameongeza "Sisi kama wizara tutachukua mawazo yake lakini endapo uwanja wa Dodoma utakamilika kabla ya mwaka 2019 basi tutaangalia kwa namna gani uwanja huo utaweza kutumika. Tukumbuke uwanja huo unajengwa kwa hisani ya Mfalme wa Morrocco hivyo hatuwezi tukampa 'deadline'.