Jumatatu , 27th Jun , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba Mama Anna Mkapa, ndiyo mtu wa kwanza kumwambia kama anafaa kuingia kwenye siasa, alipomwita kupanda gari lake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 27, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko wa fursa sawa kwa wote.

"Nikiwa ndani ya gari lake (Mama Anna Mkapa) akaniambia Samia nimekuona, wewe ni mwanasiasa mzuri sana, sasa uchaguzi unaokuja ungejaribu, nikamuambia Mama mimi sijui watu wanaingiaje huko, akaniambia we uliza tu, yale maneno yakanikaa kichwani, nilivyojaribu kweli nikaingia, safari imenifikisha hapa, nguvu ya kuingia ni maneno ya Mama Mkapa, ambaye alinichukua kwenye gari yake na nadhani Mungu alinifanya nizubae nikimbiwe ili niingie kwenye gari nikapate nguvu," amesema Rais Samia