Raila awataka wafuasi wake wagome kwenda kazini J3

Sunday , 13th Aug , 2017

Kiongozi wa Muungano wa Upinzani, nchini Kenya, Nasa, Raila Odinga amefanya mkutano wake wa kwanza wa kisiasa tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi nchini humo siku ya Ijumaa.

Aliyekuwa mgombea ubunge Kenya Raila Odinga

Katika mkutano wake huo mtaa wa Kibera, jijini Nairobi, Bw. Raila amewaambia wafuasi wake wasiende kazini kesho akisema, Muungano huo utatangaza hatua watakayochukua Jumanne ijayo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star, kiongozi huyo pia anatarajiwa kuitembelea familia ya binti wa miaka kumi aliyeuwawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya kupinga matokeo katika kitongoji cha Mathare, ambapo pia maandamano yalishuhudiwa maeneo ya Nyanza, Mathare na Kibera ambako watu wengine 10 wameuwawa.

Hata hivyo Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiang'i, amedai kutokuwa na taarifa za mtu yeyote kuuwawa kwa kupigwa risasi nchini humo, na kwamba huo ni uvumi

Kenya leo imeshuhudia utulivu baada ya vurugu hizo za Jumamosi, wakati Bw. Raila akikabiliwa na shinikizo kutoka Jumuiya ya Kimataifa kuyakubali matokeo ya uchaguzi.

Recent Posts

Current Affairs
Rais Mugabe atumbuliwa

Msanii Irene Uwoya.

Current Affairs
Uwoya otokwa povu kisa mtoto

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.

Current Affairs
Serikali kuvunja nyumba zilizojengwa bila kibali