Alhamisi , 26th Nov , 2020

Raia wa Uganda Noah Mukobe, amehukumiwa kulipa faini ya shilingi laki sita kwa kila kosa au kwenda jela kwa mwaka mmoja, baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili ikiwemo kuingia nchini bila kibali.

Pichani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Hukumu hiyo imetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Dar es salaam.

Awali, akisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Godfrey Ngwijo, alidai, Novemba 24, mwaka huu mshtakiwa alibainika na makosa mawili ambayo ni kuingia nchini bila kibali na baada ya hapo aliishi bila kibari eneo la Ubongo jijini Dar-es-Salaam.

"Nimekiri makosa kwa sababu naipenda Tanzania na kuna ndugu zangu wako hapa na nampenda Rais John Pombe Magufuli kwa sababu kaikomesha corona"  amesema mshtakiwa

Hata hivyo Mshtakiwa amefanikiwa kulipa faini yote na kuepuka kifungo cha mwaka mmoja.