Jumatano , 22nd Feb , 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana raia14 wa kigeni wenye asili ya Asia baada ya kusomewa mashtaka 3 mahakamani hapo ya kufanya kazi kinyume cha sheria katika kampuni ya Quality Group Company iliyopo hapa nchini Tanzania.

Raia wa India wakiwa Mahakamani leo

 

Akisoma mashataka matatu yanayo wakabili watuhumiwa hao 14, wenye asili ya Asia, mbele ya Hakimu Mkazi Mkeha Syprian, wakili wa Serikali Kagome Method ameeleza, mahakamani hapo kuwa washtakiwa wote 14 siku ya tarehe 13 Februari 2017, katika Manispaa ya Ilala walikutwa na maofisa uhamiaji wakifanyakazi kinyume na sheria za nchi.

Shtaka la kwanza ni pamoja na kumiliki vibali vya ukazi yaani viza za kughushi, shtaka la pili ni kuwepo nchini isivyokuwa halali na shtaka la tatu ni kufanya kazi kama washauri katika kampuni ya Quality Group kinyume cha sheria za ajira za kazi kwa wageni.

Hakimu Mkeha Syprian amewaachia watuhumiwa hao kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja huku wadhamini wao na wakitakiwa kuweka bondi ya shilingi milioni 5, kesi hiyo itaendelea tena Machi 21 mwaka huu.