Jumatano , 24th Mei , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017.

Prof. Sospeter Muhongo

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.