Alhamisi , 16th Feb , 2017

Posho ya vikao ya mbunge wa Singida Magharibi Mh. Elibariki Kingu, imetumika kuanzisha ujenzi wa zahanati nane katika jimbo hilo, ikiwa ni njia ya kutekeleza uamuzi wake wa kutochukua posho hizo, na badala yake akitaka ziwatumikie wananchi.

Mbunge Elibariki Kingu akiwa na wananchi wa jimboni kwake

Mbunge huyo amebainisha hilo mapema wiki hii alipokuwa kweye kipindi cha East Africa Breakfast, ambapo pamoja na mambo mengine alitakiwa kueleza endapo anajua matumizi ya mgao wake wa posho za vikao vya Bunge, kwa kuwa wakati Bunge la 11 likianza, alikuwa ni mmoja kati ya wabunge waliotangaza kukataa kuchukua posho hizo.

Katika majibu yake Kingu alibainisha ilishindikana kuacha kuchukua posho hizo kwa kuwa, kwa mujibu wa utaratibu wa Bunge, ni lazima asaini kuzichukua, lakini akaamua kuwa yeye binafs asitumie hata shilingi, na badala yake zikatatue kero ya zahanati jimboni kwake.

Vyumba vya madarasa katika jimbo hilo

Mbali na zahanati, Kingu amesema pia kuwa kwa kutumia posho hiyo, ameweza kuanzisha shule mpya za msingi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Winduwindu kata ya mwaru, Mtakuja kata ya Mwaru, Mtakuja kata ya Mtunduru, Mwankalaja kata ya Mgungira, Mfumbuwahumba kata ya Ighombwe kata Minyughe na Kinyarimi kata Minyughe.

Msikilize hapa akitaja matumizi ya posho yake........