Ijumaa , 25th Sep , 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, ametoa rai kwa vile vyama vya upinzani vinavyotaka kuungana ili viweze kusimamisha mgombea mmoja wa urais, visingoje hadi Oktoba 3,bali viungane hata sasa hivi ili waje waione nguvu kubwa ya CCM kwa Watanzania.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Hamphrey Polepole.

Polepole ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 25, 2020, jijini Dodoma, wakati akitoa tathmini ya kampeni za uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho.

"Mimi natoa rai wasisubiri Oktoba 3 ili waungane, hawa waungane sasa halafu ndiyo watajua tulipotoka na tulipofika na Watanzania, sisi tumeingia nchi hii ni maskini huyu mzee Magufuli kapambana leo sisi ni nchi ya uchumi wa kati", amesema Polepole.

Aidha Polepole akimzungumzia mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama ACT wazalendo amesema, "Yule mgombea wa chama cha bwana Zitto kule Zanzibar tutamshinda katika namna ambayo watu wake wa karibu wakae naye karibu, kwa sababu ushindi wa kipindi hiki utakuwa ni mkubwa mno kiasi kwamba wakae karibu  kumtia moyo".