Ijumaa , 25th Sep , 2020

Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi,(CCM), Humphrey Polepole amewajibu waliokuwa wanahoji kuhusu ujenzi wa viwanja vya ndege na ununuaji wa ndege na kusema kuwa ujenzi huo ni fursa ya kibiashara kwa watanzania.

Amesema hayo leo Septemba, 25, akiwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma,na kusema serikali ina mpango wakujenga viwanja vya ndege kwenye mikoa mingine ilikuinua uchumi na kuzidi kutengeneza fursa za kibiashara.

"Viwanja vingi vya ndege vimeboreshwa , Yote hii ni kuifungua nchi ya Tanzania kuwafungulia fursa watanzania ili waweze kusafiri kwa haraka wapeleke bidhaa na mizigo na wakaone wenza wao” alisema polepole

Aidha amesema kuwa kipindi Rais Dkt. John Mgufuli alivyoingia madarakani kulikuwa na ndege moja tu.”Wakati  Magufuli anaingia madarakaini Air Tanzania ilikuwa na kadege kadogo kabovu kamoja sasa hivi tunazitafuta ndege 11