Jumapili , 27th Sep , 2020

Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole aelezea yaliyomsibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa, marehemu Emmanuel Polycupy Mlelwa hadi kukutwa na mauti huku akilitaka jeshi la polisi kuendelea kufuatilia tukio hilo.

Marehemu Emmanuel Polycupy Mlelwa.

Akiwa kwenye mkutano wake na waandishi  leo Septemba 27, Polepole amesema kuwa  Chama cha Mapinduzi kimefuatilia jambo hilo kwa uchungu mkubwa.

Tunafahamu, sitaki kusema ili nisiingilie upelelezi wa polisi wamefanya mawasiliano na huyu kijana, wameomba kukutana naye, wakamteka, wamepotea naye tumekuja kukuta mwili wa kijana huyu eneo la Kibwena bwawani, amepigwa ameumizwa, amepoteza maisha yake" alisema Polepole

Aidha Polepole ametoa rai kwa jeshi la polisi  kufanya upelelezi huku akisema  kuwa hawako tayari kufanya siasa kwenye nchi hii inayomwaga damu.

Sisi CCM tumefuatilia natunatoa rai kwa jeshi la polisi tafadhali wakati mwingine upelelezi unachukua muda bila sababu ya msingi, kipindi hiki ukweli unajulikana hatuko tayari kufanya siasa katika nchi hii tunamwaga damu nakupoteza maisha ya watanzania akiwemo kijana huyu mdogo” alisema Polepole