Jumapili , 15th Jan , 2017

Kata zote kumi na nne katika jimbo la Pangani mkoani Tanga zimefanikiwa kupata umeme kupitia juhudi zilizofanywa na mbunge wa jimbo hilo Mhe. Juma Aweso akishirikiana na wizara ya nishati na madini.

Aweso alikuwa akizungumza kupitia Kipindi cha Weekend Breakfast cha EA Radio, amesema baada ya suala hilo la umeme kufikia pazuri, hivi sasa kilio cha wana Pangani ni huduma ya uhakika ya usafiri wa majini utakaounganisha jimbo la Pangani na maeneo mengine ya ukanda wa mwambao nchini.

Amesema mkakati wake kama mbunge hivi sasa ni kuhakikisha panakuwa na boti ya haraka (Fast Boat) kwa ajili ya huduma za usafiri katika mto Pangani itakayorahisisha 

 

Jumaa Aweso - Mbunge wa Pangani

Mbali ya mafanikio katika suala la miundombinu ya umeme na barabara, jimbo hilo pia limefanikiwa kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa mujibu wa Katibu wa Wafugaji wilaya ya Pangani Bw. Christopher Benedict Molam aliyefanya mazungumzo na Kurasa ya EATV.

Molam ametaja mbinu waliyoitumia kumaliza migogoro hiyo kuwa ni kwa kuwaelimisha wafugaji kuwa huwezi kula nyama peke yake pasipo kuhitaji mahindi na aina nyingine za mazao huku wakulima nao wakielimishwa umuhimu wa mifugo kama kitoweo muhimu kwao kwani hakuna anayeweza kula mahindi pasipo kuhitaji nyama ambayo inatokana na mifugo.