Jumamosi , 16th Sep , 2017

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga mjini Kigoma imeungua moto jioni ya leo ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika.

Hayo yamethibitishwa na Afisa habari wa chama cha ACT, Abdalla Khamis na kusema ni kweli tukio hilo limetokea lakini siyo katika nyumba ambayo anaishi Mbunge Zitto Kabwe.

"Ni kweli nyumba ya Zitto imeungua moto jioni ya leo lakini siyo nyumba ambayo anaishi yeye binafsi, bali ni nyumba ambayo imejengwa katika kiwanja kimoja na nyumba anayoishi kwa sasa", amesema Abdalla.

Taarifa kamili tutaendelea kukujuza.