Jumatatu , 19th Oct , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewataka viongozi wa vyama vya siasa kutoa Elimu kwa wanachama wao kwa kuzingatia na kutekeleza sheria ya uchaguzi ,Maelekezo na kanuni za tume hiyo ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanya kwa amani na utulivu.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva.

Hayo yamesemwa na kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Bi. Asina Omary wakati akiwasilisha taarifa kwa umma kuhusu maelekezo ya mambo yasiyoruhusiwa kufanyika siku ya kupiga kura katika mkutano na vyama vya siasa mkoani Shinyanga.

Bi. Asina amesema kuwa Vyama vya siasa vina nafasi kubwa ya kutumia majukwaa ya kisiasa kuanza kumasisha na kuelemisha juu ya sheria ya Uchaguzi na mambo ambayo hayatakiwi kufanywa siku ya uchaguzi ikiwemo kuvaa nguo za vyama.

Kwa upande wa kaimu mkuu afisa uchaguzi kanda ya kati Bi. Martina Magaula amewataka wananchi kuepuka kuvaa sare za vyama au kufanya kampeni katika vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi mkuu utakaofanya Oktoba 25.