Jumanne , 18th Aug , 2020

Tume ya Taifa ya uchaguzi imesema ni muhimu kwa Vyombo vya habari kuhamasisha wananchi kujua kuhusu Elimu ya mpiga kura ili wawe na uwezo kuwapima wagombea Sambamba na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 28,2020.

Akitoa Rai hiyo katika kikao Cha pamoja Kati ya Tume hiyo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji mstaafu Semstocles Kaijage amekiri kuwa wanahabari Wana nguvu kubwa ya kuhamasisha kwa haraka zaidi hivyo kuwaomba kutumia vema karamu zao hasa katika kipindi hiki Cha kuelekea  uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo amesema watahakikisha kuwa Kama Tume wanasimamia uchaguzi huu kwa kutoa fursa sawa ili kupitia Maadili yaliyofikiwa na wadau wa Uchaguzi yanafuatwa na kutoa nafasi kwa majimbo yote 264 na kata 3959 kwenye vituo vyote vyauchguzi  80,185 vinakamilisha zoezi kwa Amani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa uchuguzi kutoka katika Tume Dkt Charles Mahera wakati akiwasilisha mada kwa wahariri amesema maboresho mengi yamefanyika huku tume ikitoa zaidi ya vibali 240 kwa asasi ili kuendelea kutoa Elimu ya mpiga Kura.