Jumamosi , 21st Oct , 2017

Ndege moja inayodaiwa kuwa ni ya mmiliki binafsi iliyokuwa imebeba wanasiasa nchini Kenya imeanguka katika Ziwa Nakuru nchini humo.

Taarifa kutoka kwa Mwandishi wetu amesema kwamba Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na serikali ya nchi hiyoimesema kwamba wealiokuwepo ndani ya ndege hiyo ni wanasiasa wa Jubilee ambao walikuwa wakienda kufanya kampeni

Haijabainika ni wanasiasa wa Kiwango kipi ambao walikuwepo ndani ya ndege hiyo iliyoanguka.

Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari naMkuu wa kukabiliana na majanga haijasema chanzo kilichosababisha ndege hiyo kuanguka.

Hata hivyo inadaiwa kwamba nchi hiyo tangu usiku wa kuamkia leo kulikuwa na mvua kubwa.

Msemaji wa serikali anatarajiwa kuzungumza kutoa taarifa kamili pamoja na idadi ya hao wanasiasa.

Taarifa kutoka Seneta wa Nakuru Bi Susan Kihika baadhi ya waliokuwepo kwenye helikopta hiyo walikuwa ni timu yake ya mawasiliano.

Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa Taarifa zaidi.