Jumanne , 14th Feb , 2017

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka, wadau wa sheria kote nchini kutoa mapendekezo ya kuundwa kwa kanuni za kisheria zitakazosimamia vyama vya siasa na wanasiasa mara uchaguzi unapomalizika.

Dkt. Harrison Mwakyembe

Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Amesema, Tanzania haina sheria wala kanuni zinazo wadhibiti na kuwasimamia wanasiasa kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao jambo ambalo limekuwa likileta mvutano akitolea mfano zuio la kuendesha shuguli za kisiasa nchini hadi uchaguzi wa mwaka 2020 ambao unalalamikiwa na vyama vya upinzani.

Mtazame hapa......................