Alhamisi , 23rd Mar , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.

Katika Mabadiliko hayo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Uteuzi huu unaanza mara moja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu , haijaelezwa endapo Nape Nnauye ameteunguliwa uteuzi wake ama la

Wateule wote wataapishwa kesho Mchana tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu, Jijini Dar es Salaam.