Jumapili , 20th Aug , 2017

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego amesema ataandaa mafunzo maalumu ya ukakamavu kwa ajili ya watendaji wote wa serikali mkoani humo wakiongozwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya kuwaweka imara viongozi hao.

Akizungumza mkoani humo, Dendego amesema wapo baadhi ya watendaji ambao wanabweteka katika utendaji kazi, hivyo kupitia mafunzo hayo anaimani watapiga kwata la maendeleo kwa wananchi wanaowaongoza.

"Viongozi wote nitawaandalia mafunzo maalumu, Tukafungiane tukapige kwata na tukirudi tupige kwata la maendeleo. Wale ambao walipita jeshini wao wataji-brush tu" alisema

Aidha, mkuu huyo wa mkoa akaeleza dhamira yake ya kubuni vazi la kizalendo la mkoa huo ambalo litavaliwa na viongozi wote wa serikali katika siku zote za kazi ili kuwarahisishia wananchi kuwatambua viongozi wao.

Oktaviani Lepembile ni afisa tarafa wa Mtwara mjini, anaeleza namna alivyopokea mapendekezo hayo ya mkuu wa mkoa.

Sikiliza hapa chini akifafanua zaidi.