Msafara wa Sumaye wazuiliwa

Monday , 19th Jun , 2017

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani (CHADEMA), leo amezuiliwa na polisi kuendelea na msafara wake katika ziara ya kutembelea na kujionea utendaji wa kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA.

Meya wa Ubungo Mhe. Boniface Jacob akitoa akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda wa Pwani.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene inasema kuwa kiongozi huyo ambaye alikuwa ameambatana na viongozi wengine wa Chama, madiwani wa CHADEMA wamezuiliwa na jeshi la polisi maeneo ya Halmshauri.

"leo Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Mhe. Frederick Sumaye akiongozana na viongozi wa chama na madiwani wa CHADEMA, alikuwa na ziara ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA. Katika hali ambayo haijatolewa sababu zozote za msingi, baada ya Mhe. Sumaye pamoja na viongozi wengine kupata taarifa fupi kutoka kwa Meya Boniface Jacob ofisini kwa Meya na walipokuwa wakitoka kuanza ziara, msafara wao umezuiwa na polisi maeneo ya Ofisi za Halmashauri ambapo OCD amemuomba Meya afike kituoni kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala kadhaa kwa muda usiozidi dakika 10" alisema Tumaini Makene. 

Recent Posts

Simon Msuva na Haruna Niyonzima

Sport
Msuva amlilia Niyonzima

Makamu wa Rais Samia Suluhu

Current Affairs
Serikali yetu haitarudi nyuma - Samia

Rais Magufuli.

Current Affairs
Rais Magufuli awachimba biti wanafunzi

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa

Sport
Mkwasa kuwashika koo waliochoma jezi

Msanii Dogo Janja Kushoto, na Kulia ni Mfanyabiashara Muna Love

Entertainment
Dogo Janja aruka kwa Muna Love