Alhamisi , 29th Oct , 2020

Katika uchaguzi huu Chama Cha Mapinduzi (CCM) miongoni mwa wagombea wake wa ubunge nchi nzima pia walikuwemo wagombea watatu  wa ubunge ambao walitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika miaka ya mwanzoni na wengine dakika za lala salama bunge likiwa linaelekea kuvunjwa,

Pichani ni Wabunge wateule kwa tiketi ya CCM, Kushoto ni Godwin Mollel (Siha), Mwita Waitara (Tarime Vijijini), Kulia ni David Silinde (Tunduma)

 kuvunjwa ambao ni Mwita Waitara, Godwin Mollel na David Silinde.

Kwa upande wake David Silinde hapo awali alikuwa Mbunge wa jimbo la Mbozi Mjini tangu 2010  kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kuhamia CCM na kupitishwa kuwania ubunge aligombea jimbo la Tunduma ambapo ameibuka msindi kwa kura 43,276 dhidi ya mshindani wake Frank Mwakajoka wa CHADEMA aliyepata kura 12,433.

Aidha kwa upande wa Dkt Godwin Mollel yeye aliingia Bungeni mwaka 2015 na mwaka 2017 alikihama chama chake ''CHADEMA'' na kutimkia CCM, Disemba 2017 akiwa sehemu ya kuunga mkono juhudi zilizokuwa zikifanywa na serikali ya awamu ya tano, katika uchaguzi mdogo uliofanyika Februari 2008 Mollel aliibuka mshindi kwa kupata kura  25,611 huku Elvis Mosi wa CHADEMA akipata kura 5,905 na katika uchaguzi Mkuu huu amepata kura 22,172, akifuatiwa na Elvis Mossi wa CHADEMA aliyepata kura 8614.

Kwa upande wake Mwita Waitara alichaguliwa kuliongoza Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2015, alijiuzulu na kujiunga na CCM mwezi Julai 2018 na baada ya siku 4 tangu kuapishwa kwake bungeni Waitara aliteuliwa na Rais John Magufuli  tarehe 10 Novemba 2018 kuwa Naibu waziri wa TAMISEMI katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.