Jumatatu , 25th Sep , 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu leo amefungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umezinduliwa leo Septemba 25, 2017 ambapo utafanyika kwa siku tatu ukiwa na kauli mbiu isemayo “Mahakama Madhubuti inayowajibika na Jumuishi”, pia kutakuwa na mada mbalimbali kutoka kwa viongozi ambao ni Majaji na mahakimu.

Makamu wa Rais amewakaribisha wageni wote na kuwasihi wawe huru kuendelea na serikali iko pamoja nao katika muda wote wa mkutano huo.

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanzania, Ignas Hatusi amesema kuwa Mkutano huo una lengo la kujenga Mahakama shirikishi, Mahakama inayowajibika na Mahakama Dhabiti kiutendaji kwa kuimarisha utendaji wa taasisi za kimahakama.

Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki wapatao 354 wakiwemo 13 ambao ni Marais na Majaji kutoka Austaria, Zambia, Afrika Mashariki na Pakistani.